RC MWAMBUNGU AWAFUNDA WATENDAJI MADABA
NA STEPHANO MANGO,MADABA
MKUU wa
mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewataka watendaji wa vijiji na kata wa
mkoani humo kuhakikisha wanawafuatilia kikamilifu wanufaika wa mfuko wa
maendeleo ya jamii Tasaf na kuwachukulia hatua wale wote ambao wametumia
fedha hizo kinyume na malengo yaliyokusudiwa na
serikali.
Mwambungu aliyasema hayo jana wakati alipo kuwa akizindua baraza jipya
la madiwani katika Halmashauli ya Madaba mkoani hapo ambayo imeanzishwa
hivi karibuni na imekuwa na madiwani wa kata nane na vitimaalum wa tatu
na mbunge na kufanya jumla ya madiwani 12.
Kwa mjibu wa mkuu
huyo akitoa maagizo hayo alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya watu hasa
akinababa kutumia vibaya fedha zinazotolewa naTasaf kwa madai kuwa
serikali imewapatia watumie watakavyo jambo ambalo siyo kweli .
Alisema kuwa serikali imeamua kuziangalia kaya masikini ili
kuwanusuru na hali hiyo lakini bado baadhi yao hawaoni jitihada
zinazofanywa na serikali na badala yake wamekuwa wakitumia misaada hiyo tofauti na malengo yaliyokusudiwa.
“Nawaagiza watendaji kwa kuwa ninyi ndiyo mnaishi na kaya hizo na
mnaziona zinavyotumia vibaya misaada hiyo hivyo ni vema mkazikamata na
kuwaweka ndani ili iwe funzo kwa watu wengine ambao wanatumia vibaya kwa
kujificha”alisema mkuu wa mkoa.
Kwa upande wake mmoja
aliyeteuliwa kushughulika na mambo ya Tasaf katika baadhi ya vijiji vya
halmashauri ya Madaba Vumilia Tawete akizungumza na gazeti hili
kijijini hapo alisema kuwa kunabaadhi ya wanufaika bado hawana elimu ya
kutosha kuhusiana na misaada hiyo hivyo ni vema kabla ya kuwagawia
watalaam wauchumi watoe somo kwa walengwa namna ya matumizi ya fedha
hizo.
Tawete alisema kuwa chamoto hizo tunakutana nazo kwa
kuwaona baadhi yao hasa wakinababa akishapokea fedha anapitia moja kwa
moja kwenye vilabu vya pombe huku wengine wakitoa maneno ya kejeli kuwa
serikali imeamua kuwalipa mishara na watu ambao ni masikini.
Naye mbunge wa jimbo hilo Joseph Mhagama akimwelezea mkuu wa mkoa
alisema kuwa licha ya maagizo ya kuwachukulia hatua watu hao lakini
jimbo lake limejipanga vema kukabiliana na watumishi wazembe ambao
wanafanya kazi kwa kutaka maslai.
Katika baraza hilo lilifanya uchaguzi
ambao mgombea wa CCM Vastus Mfikwa hakuwa na mpinzani hivyo alishinda
kura zote 12 kwa kuwa halmashauri hiyo haina madiwani wa vyama vya
upinzani huku mwenyekiti huyo akiahidi kufanya kazi za wananchi kwa
kufuata kasi ya mheshimiwa
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Magufuli.
MWISHO.
Category:
0 comments